Forum

Notifications
Clear all

Fahamu bunduki 5 hatari za Sniper zinazotumiwa na nchi zenye makali ya kijeshi

(@dukuzumurenyi)
BlackStonishing Kmty Registered Registered

Fahamu bunduki 5 hatari za Sniper zinazotumiwa na nchi zenye makali ya kijeshi

Yusuf Jumah

BBC Swahili

Saa 4 zilizopita
 
Saa 4 zilizopita
ik

CHANZO CHA PICHA,WIKIPEDIA

Ni bunduki ambazo umeziona katika filamu au hata kwenye runinga katika maeneo yenye vita .

Wengi hutamai sana kufahamu mengi kuhusu bunduki hizi za msafara marefu ambazo wanaofuatilia zinavyotumiwa hasa katika vita wanafahamu jinsi zilivyo hatari .

Lakini kando na kupewa mafunzo ya kipekee kuweza kuitumia ,unafaa kujua kwamba bunduki hizo za sniper ni nyingi na kuna nyingi ambazo zinatengezwa na kuboreshwa .

Miongoni mwa bunduki hizi za sniper , hizi tano kutoka Uingereza ,Marekani na Urusi zinafahamika kwa uwezo wake mbali mbali ingaaje bado kuna nyingi ambazo hazimo katika orodha hii ambazo ni hatari .

Sniper ni askari aliyefundishwa haswa katika ugumu wa vita, ambaye kwa ustadi kamili amejifunza ustadi wa kipekee katika ulengaji wa shabaha .

Sniper hujificha katika maeneo mbali mbali ikiwemo juu ya paa za nyumba, na vichakani. Lengo lake kuu ni uharibifu mkubwa kwa adui iwezekanavyo,.

Katika mizozo mingi ya kivita umewahi kuona bunduki inayoonekana tofauti na nyingine ambayo hutumiwa kulenga mbali .Bunduki hizo za sniper huwa za miundo mbali mbali na zimetengezwa katika nchi tofauti. Huko mashariki ya kati kuna makundi ambayo yamewapa mafunzo kabambe askari wake waaotumia bunduki hizo na Marekani ,Urusi na Uingereza ni miongoni mwa nchi zenye vikosi maalum vinavyotumia bunduki hiyo ya masafa marefu .

Maono mazuri, uvumilivu, na uwezo wa kushughulikia silaha ni ujuzi wa kimsingi kwa sniper. Lakini ujuzi huu wote hauna maana kabisa ikiwa mpiganaji hana bunduki nzuri.

Tumeandaa maelezo kuhusu bunduki 5 za hali ya juu zinatumiwa kwa kulenga mbali ambazo zinatumiwa na nchi hizi na hata kuuzwa katika mataifa yasio na uwezo wa kuzitengeza .

5 - US CheyTac M200 Intervention

Hii ni silaha ya risasi kubwa na nzito iliyotengenezwa katika miaka ya 2000 huko Marekani.Iliundwa kushinda adui kwa umbali wa hadi 2 km. Wakati wa kuijaza risasi utalazimika kufanya hivyo mwenyewe na sio moja kwa moja .

ik

CHANZO CHA PICHA,WIKIPEDIA

Haina kifaa cha darubuni ili kuweza kuona mbali wakati wa kulenga lakini ina uwezo wa kupachikwa vifaa vya kukuwezesha kuona mbali wakati unapoitumia ama kulenga.

Kwenye pipa lake la kuvurumisha risasi , unaweza kufidia uzito wake unapoitumia kwa kuweka silencer inayozuia kelele. Imetengezwa kwa vifaa maalum vya glasi ya fibre iliyokausha kwanza .Bunduki hii imekiuwa ikitengezwa tangia mwaka wa 2001 .

4 - Russian Orsis T-5000

Bunduki inayoshikilia nafasi ya nne katika ukadiriaji huu ni hii iliyoundwa na kampuni binafsi ya Urusi ya Promtekhnologii.

Bunduki hii inafahamika kwa kujifunga kwa urahisi kwa awamu mbili .Ni mojawapo ya bunduki hatari zaidi za masafa marefu na inaminika kuuzwa kwa nchi mbali mbali .

uj

CHANZO CHA PICHA,WIKIPEDIA

Pipa lake la kuvurumisha risasi limetengenezwa na chuma, bunduki imeundwa kwa kutumia teknolojia ya upangaji ya tapestry.

Nguvu inayohitajika kupunguza ndoano inaweza kubadilishwa ndani ya gramu 600-900 au kilo 1-1.5, yote inategemea toleo la kichocheo chake

Inaweza pia kuinuliwa kwa maguu mawili ili kutumika katika hali inayolazimu iinuliwe kidogo

3 - US Barrett M82

Hii ni bunduki kubwa ya sniper iliyotengenezwa na kampuni hiyo chini ya jina Barrett Firearms . Inatofautiana na silaha za kawaida za sniper kwa kuwa inaweza kuhimili teknolojia nzuri na kudhoofisha risasi za adui kutoka umbali mkubwa na salama. Hii inaweza kufanya uharibifu zaidi kwa maadui kuliko kurusha risasi kutoka mbali.

ju

CHANZO CHA PICHA,WIKIPEDIA

Pipa ni la kustahimi hali ya baridi, lina breki ya mdomo wa mtutu na kamera mbili za za kipekee . ina uwezo wa kujisamamia katika kupunguza joto lake wakati inapotumiwa kwa muda mrefu .

Ina maguu matatu ya kuiweka juu na bunduki hii pia inaweza kutumika kwa magari yanayobeba bunduki APC wakati wa vita .

2 - British Accuracy International AW50

Bunduki hii kubwa ya Uingereza ina uwezo wa kuzunguka kuangalia upande wowote na wakati unapoitumia hulazimiki kuamka ili kuielekeza unakotaka .

ju

CHANZO CHA PICHA,WIKIPEDIA

Upeo wa juu na bunduki ni kilomita 2, na inaweza kuhifadhi hadi raundi tano za risasi zinazofyatuliwa kwa mfululizo .

Kwa sasa, bunduki hiyo inatumiwa na vikosi maalum katika majeshi ya Australia na Uingereza.

Usahihi wake wa hali ya juu umeifanya kuwavutia wengi na inatumika sana katika mizozo inayohitaji bunduki zenye uwezo kama wake kupambana na maadui .Kuna vikwazo kuhusu makundi yanayoweza kuuziwa bunduki hii lakini bado imejipata katika mikono ya watu wasiohitajika kuwa nayo.

1 - British L96A1

Bunduki hii ni mfano wa nguvu ya usahihi na na hatari . Iliundwa nchini Uingereza mnamo 1982 na hadi leo ipo katika kiwango cha kipekee .

Kutoka kwa bunduki hii, rekodi ya ulimwengu iliwekwa kwa lengo la risasi lililofika -mita 2475.

ju

CHANZO CHA PICHA,WIKIPEDIA

Umbali wa kushangaza cha kupiga risasi ni 1.5 km. Thamani ya soko ya bunduki hii ni karibu dola elfu 10.

 

 

https://www.bbc.com/swahili/habari-58103343?at_medium=custom7&at_campaign=64&at_custom1=%5Bpost+type%5D&at_custom2=twitter&at_custom3=BBC+Swahili&at_custom4=70E124CE-F5E6-11EB-B688-343116F31EAE

Quote
Topic starter Posted : 05/08/2021 12:29 pm
Share:

June 16th the Kambon family had a major family emergency.  Dr. Kambon’s wife Kala and children were involved in a serious car accident and admitted to the hospital.   All are doing well and recovering.

The family’s only mode of transportation was totaled in the accident.

We are asking for the support of Abibitumi family to assist the Kambon family during this trying time.    

X
X
X
X