-
1. Faida/tijara/kivuno/chumo/ziada (profit) – Pato libakialo baada ya kuondoa gharama za kufanya biashara k.v. ununuzi na usafirishaji. (Income gained after deducting costs of doing business like procurement and transportation)
2. Hasara (loss) – Ukosefu wa faida; Hali ya kupoteza pato au mali katika biashara. (Lack of profit; state of losing income or material in a business)
3. Bei (price) – Kiwango cha pesa cha kununulia au kuuzia bidhaa au huduma fulani. (Amount of money used for buying or selling a good or service)
4. Uuzaji wa rejareja (retail trade) – Uuzaji wa kiasi kidogo kidogo. (Selling in small quantities)
5. Uuzaji wa jumla (wholesale trade) – Uuzaji wa kwa pamoja. (Selling in bulk)
7. Raslimali (resources) – Ujumla wa mali yaanyomilikiwa na mtu au nchi. (The sum of materials owned by a person or nation)
8. Malighafi (raw materials) – Mali yanayotumika kutengeneza vitu vingine k.m. pamba ni malighafi ya kutengenezea nguo. (Materials used to make other things e.g. cotton us a raw material for making clothes)
9. Maliasili (natural resources) – Utajiri kama vile madini, misitu, maziwa, mito, anga vinavyopatikana katika mazingira. (Riches like minerals, forests, lakes, rivers, atmosphere as found in the environment)
10. Uwekezaji (investment) – Kutumia pesa/mali ili kuzalisha fedha/mali zaidi. (Using money/materials in order to create more money/materials)