• 10,006 Abibisika (Black Gold) Points

      Angahewa ya dunia:
      Mbali na kutuandalia hewa ya kupumua, blanketi inayotuzunguka ya gesi mbalimbali hutupa ulinzi. Tabaka la nje la angahewa, linaloitwa tabakastrato, lina oksijeni ya aina fulani inayoitwa ozoni, ambayo hufyonza asilimia 99 ya miale hatari ya urujuani. Kwa hiyo, tabaka la ozoni hulinda aina nyingi za viumbe dhidi ya miale hatari. Kiwango cha ozoni kwenye tabakastrato hubadilika kulingana na ukali wa miale ya urujuani. Kubadilika huko huifanya kuwa ngao murua.

      Angahewa pia hutulinda dhidi ya vifusi vinavyoanguka kila siku kutoka katika anga la nje—mamilioni ya vitu, vidogo kwa vikubwa. Vingi kati ya vitu hivyo ni vimondo, ambavyo huteketea vinapoingia kwenye angahewa la dunia, vikitokeza nuru angavu. Wakati huohuo, ngao za dunia hazizuii miale ambayo ni muhimu kwa uhai, kama vile ile inayotokeza joto na nuru. Angahewa hutupatia joto duniani vizuri, na wakati wa usiku huhifadhi joto kama blanketi.

      [The atmosphere:
      Apart from preparing our breathing air, the blanket of various gases that surrounds us protects us. The outer sphere of the atmosphere known as stratosphere, has a type of oxygen known as ozone which absorbs 99 percent of harmful ultraviolet radiation. Through that, the ozone layer protects many types of creatures from harmful radiation. The level of ozone in the stratosphere changes according to the intensity of ultraviolet radiation. Those changes make it a more effective shield.

      The atmosphere also protects us from debris that fall everyday from space—millions of things, big and small. Most of those things are meteors, which burnout upon entering the atmosphere, giving off bright light. Simultaneously, the earth’s shields do not block radiation that is important for life, like those that give us heat and light. The atmosphere gives us heat on earth very well, and at night conserves heat like a blanket.]