-
Chui hunyatia windo lake kimyakimya na kisha humrukia, na kumnyonga koo lake kwa kumng’ata haraka. Chui kwa kawaida huficha mawindo yao kwenye vichaka vilivyoshona au huyachukua mpaka juu ya miti, na wana uwezo wa kubeba wanyama hata wenye uzito mara tatu ya uzito wao. Chui ndiye mnyama pekee miongoni mwa jamii ya paka anayeweza kubeba mawindo yake juu ya miti. Uchaguzi wa mawindo kupitia tafiti umeonekana kuzingatia hali fulani ikiwemo ukubwa wa kundi analokuwemo mnyama awindwaye, ukubwa wa pori na mazingira yasiyoweza kuhatarisha maisha ya mwindaji – chui.
(The Leopard creeps silently towards its prey then jumps on it and clutches its throat by a quick grasp. Leopards usually hide their kill in thick bushes or take it up on trees, and they have the ability to even carry animals three times their own weight. The leopard is the only animal in the cat family that can carry its kill up a tree. The choice of prey through searching has been seen to consider particular things among which are the size of the group the prey is in, the size of the hunting field, and an environment that will not endanger the life of the hunter – leopard.)
-
A natural and clever way to hunt and devour prey.
-
Very clever and practical for a lone hunter
-
-